Mpanzu alilia Simba...
 
Notifications
Clear all

Mpanzu alilia Simba baada ya kufeli KRC Genk, hataki tena ucheza AS Vita

1 Posts
1 Users
1 Reactions
118 Views
(@elisha-mchezaji)
Reputable Member
Joined: 5 months ago
Posts: 139
Topic starter  

1725866012155.png

Inaelezwa kuwa Winga hatari wa DR Congo Ellie Mpanzu amefeli majaribio yake na KRC Genk,kwa sasa amerejea Kishansa kuangalia mustakabali wa maisha yake….ukweli ni kwamba Mpanzu hataki tena kucheza AS Vita Club,ingawa bado wanajaribu kumshawishi.

Inaelezwa kuwa Simba wapo kwenye nafasi nzuri ya kuinasa saini ya Mpanzu kama wataamua kurudi tena, ni baada ya majaribio yao mawili kutofanikiwa kipindi cha dirisha kubwa la usajili.

Rais wa AS Vital Amadou Diaby analazimisha kumbakiza mchezaji huyo ambaye Uongozi wa klab hiyo, kabla ya kwenda Ubelgiji walikuwa wamemuahidi kumlipa mshahara mkubwa zaidi atakaolipwa na Simba, huku wakipanga kumpa Unahodha wa timu.

Screenshot 2024-09-09 101412.png

Kwa upande wa Simba bado wana nafasi ya kumpata mchezaji huyo kwani kwa upande wa Mpanzu anataka kutafuta changamoto mpya, na taari alishawaaga marafiki zake wa karibu, hivyo Simba wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuinasa saini ya winga huyo katika dirisha dogo la usajili mwezi wa kwanza.

 


   
Jason de kid reacted
Quote
Share: