Hakuna ubishi juu ya kiwango kizuri kinachooneshwa na aliyekuwa mchezaji wa Yanga Fistok K,Mayele pale Pyramid mpaka sasa Mayele ni top scorer wa timu kitu ambacho kimewashitua baadhi ya timu kama Kaizer Chiefs kuhitaji kandarasi ya staiker huyo wa Pyramid huku taarifa za awali zinasema kuwa ni ngumu kwa mchezaji Mayeli kuondoka klabuni.
Huku jangwani napo imekuwa ni mshikemshike kwa staiker kinda wa Yanga naye amekuwa akihusishwa na klabu kama Kaizer Chiefs na Wydad ya nchini morocco kitu ambacho kimekuwa gumzo kuwa yanga haipo tayari kumtoa isipokuwa kwa dau wanlotaka wao.
Nimeona klabu hizi za afrika zimetupia jicho kwenye viwanja vya jangwani sababu ikiwa ni ubora wa wachezaji kama Mayele alipotoka na alipoenda moto ni ule ule hivyo umevutiwa sana na klabu za afrika kuhitaji saini za wachezaji wa Yanga.